Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania ya Wasichana chini ya miaka 20, Tanzanite Queens imefuzu fainali za Fifa za Kombe la Dunia-U20 2026 baada ya kuilaza Cameroon mabao 2-0.
Timu hizo zimeumana Jumapili Mei 10, 2026 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar na kwa matokeo hayo Tanzanite Queens imefuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya kufungwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza.
Kwa mantiki hiyo, Tanzania Queens sasa inajiandaa kwenda nchini Poland kushiriki fainali hizo zitakazofanyika Septemba mwaka huu baada ya matokeo ya jumla ya mabao 3-3 baina yake na Cameroon.
Walioisaidia Tanzanite Queens kupeperusha vyema bendera ya Tanzania ni Mary Aaron aliyefunga bao kipindi cha kwanza wakati bao la pili lilifungwa kipindi cha pili na Hasnath Ubamba.
Akizungumzia ushindi wa timu yake, kocha wa Tanzanite Queens, Bakari Shime alisema wana furaha kwa kufuzu michuano hiyo na anawapongeza wachezaji wake kwa juhudi walizoonesha hadi kufikia hatua hiyo kubwa.
Tanzanite Queens sasa inaungana na timu za Ghana na Nigeria ambazo zimefuzu michuano hiyo wakati timu nyingine itajulikana baada ya mechi kati ya Ivory Coast na Benin.
Kimataifa Tanzanite Queens yafuzu Kombe la Dunia
Tanzanite Queens yafuzu Kombe la Dunia
Read also
