Na mwandishi wetu
Nyota wa Yanga kutoka Uganda, Allan Okelo ameendelea kuwa tishio katika Ligi Kuu NBC baada ya kufunga mabao mawili wakati timu yake ikiilaza Coastal Union ya Tanga mabao 3-0.
Okello ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Uganda au Uganda Cranes, licha ya kufunga mabao hayo mawili pia ndiye aliyetoa pasi iliyozaa bao la tatu lililofungwa na Maxi Nzengeli.
Katika mechi ya ligi hiyo iliyopita dhidi ya KMC, Okelo pia ndiye aliyeifungia Yanga bao pekee na la ushindi na hivyo ameendelea kudhihirisha ubora wake akiwa hadi sasa amefikisha jumla ya mabao matano.
Ushindi dhidi ya Coastal uliopatikana leo Jumamosi Mei 9, 2026 kwenye dimba la KMC Dar es Salaam, umeifanya Yanga kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 54 katika mechi 22.
Yanga sasa wanakuwa wamewaacha mahasimu wao wa soka nchini Tanzania, Simba wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi nane.
Yanga ilianza kuandika bao lake la kwanza dakika ya 18 baada ya Okello , bao lililotokana na kazi nzuri iliyofanywa na Prince Dube aliyetoa pasi akiwa kwenye eneo la penalti la Coastal.
Okello, aliyejiunga na Yanga msimu huu wakati wa usajili wa dirisha dogo, aliongeza bao la pili safari hii akiitumia pasi ya Pacome Zouzoua kabla ya kutoa pasi iliyozaa bao la Nzengeli dakika 12 baadaye.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Singida Black Stars wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Airtel mjini Singida walitoka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mabao ya washindi yalifungwa na Ndumumwe Mosi aliyefunga mawili dakika ya 10 na 42 wakati mabao mengine mawili yalifungwa na Lamine Jarjou na Emmanuel Keyeke dakika za 52 na 67.
Kimataifa Yanga yaipiga Coastal 3-0, Okello atupia mawili
Yanga yaipiga Coastal 3-0, Okello atupia mawili
Related posts
Read also
