Madrid, Hispania
Bao la penalti la dakika za lala salama la Lucas Paqueta limetosha kuifanya Brazil itoke sare ya mabao 3-3 na Hispania katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Berbabeu.
Katika mechi hiyo ya Fifa iliyochezwa jana Jumanne, Hispania ndio walioanza kupata bao dakika ya 12 lililofungwa na Rodri kwa mkwaju wa penalti kabla Dani Olmo hajaongeza la pili dakika ya 36.
Dakika tano kabla ya mapumziko, Brazil waliandika bao lao la kwanza lililofungwa na Rodrygo na Moreira de Sousa kusawazisha dakika tano baada ya mapumziko na kufanya timu hizo ziwe sare ya mabao 2-2.
Rodri kwa mara nyingine aliifungia Hispania bao la tatu kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 86 na kufanya matokeo yawe 3-2 na hatimaye mkwaju wa penalti wa Paqueta ukatosha kuipa Brazil bao la tatu katika dakika sita za nyongeza na kufanya ubao usomeke 3-3.
England, Ubelgiji zatoka sare
Katika mechi nyingine ya kirafiki, bao la Jude Bellingham liliiwezesha England kutoka sare ya mabao 2-2 na Ubelgiji katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Wembley.
Walikuwa ni Ubelgiji walioanza kupata bao dakika ya 11 lililofungwa na Youri Tielemans lakini Ivan Toney akiichezea England kwa mara ya kwanza akasawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 17.
Ubelgiji waliendelea kupambana na kuandika bao la pili dakika ya 36 mfungaji kwa mara nyingine akiwa ni Tielemans hali iliyoiweka England katika wakati mgumu kabla Bellingham hajasawazisha katika dakika tano za nyongeza.
Matokeo ya mechi za kimataifa za kirafiki
England 2-2 Ubelgiji
Ujerumani 2-1 Uholanzi
Jamhuri ya Ireland 0-1 Uswisi
Scotland 0-1 Ireland Kask
Slovenia 2-0 Ureno
Ufaransa 3-2 Chile
Hispania 3-3 Brazil
Zambia 2-1 Malawi
Cayman Islands 0-4 Moldova
Kenya 3-1 Zimbabwe
Uganda 2-2 Ghana
Finland 2-1 Estonia
Kimataifa Brazil, Hispania hakuna mbabe
Brazil, Hispania hakuna mbabe
Read also
