Manchester, England
Kipa namba moja wa Man United, Andre Onana amesema kwamba hakuwa mwenye raha katika miezi sita ya kwanza katika klabu hiyo.
Onana alijiunga na timu hiyo katika usajili wa dirisha kubwa majira ya kiangazi mwaka jana akitokea Inter Milan kwa ada ya Pauni 47 milioni, amehusishwa na makosa kadhaa katika mechi za nusu ya kwanza ya msimu huu.
Moja ya makosa anayotajwa kuyafanya kipa huyo, ndiyo yaliyochangia timu hiyo kutolewa mapema kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ingawa amekiri kwamba kwa sasa ameanza kujiona yuko salama na mwenye amani.
“Tayari nimeshajijua mimi ni kipa wa aina gani, imenichukua miezi sita au saba kutoweza kucheza vizuri, kushindwa tu kujisikia vizuri,” alisema Onana.
“Kilikuwa kipindi kigumu kwangu, kwa sasa najiona niko sawa, wakati ule kila kitu kilikuwa kipya, ilikuwa jambo gumu kwangu kwa sababu nyingi tu, ilikuwa nchi mpya, kwa sasa najiona niko sawa, kwangu muhimu ni kuwa sawa na mwenye furaha, hapo nitaanza kung’ara,” alisema Onana.
Akiwa katika msimu wake wa mwisho na Inter Milan kabla ya kutua Man United, Onana aliiwezesha timu hiyo kufikia hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Juni mwaka jana.
Msimu huu hata hivyo mambo yamekuwa magumu kwa Man United katika michuano hiyo, timu hiyo imeishia hatua ya makundi huku Onana akibebeshwa lawama kwa makosa aliyoyafanya katika mechi dhidi ya Bayern Munich na Galatasary hadi timu hiyo kumaliza katika kundi lake ikiwa mkiani.
Kimataifa Miezi 6 migumu kwa Onana Man United
Miezi 6 migumu kwa Onana Man United
Read also
