Na mwandishi wetu
Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) limeishukuru Serikali ya Tanzania kwa kujitolea kugharamia kambi za timu za taifa za michezo mbalimbali ikiwemo ngumi.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema hayo Jumanne hii na kufafanua kuwa hatua hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao ikiwemo Tanzania kushiriki mashindano mbalimbali bila kukosa.
“Huko nyuma tulishindwa kuiweka timu hata kambini kutokana na ukata lakini tulikuwa tunakwenda kwenye mashindano na idadi ndogo ya wachezaji kwa sababu hatukuwa na uwezo wa kusafirisha wachezaji wengi lakini tangu serikali imeweka mkono wake kumekuwa na maendeleo makubwa,” alisema Mashaga.
Mashaga pia alizungumzia maandalizi yao kuelekea mashindano ya Afrika, akisema yanakwenda vizuri na wapo tayari kwa ajili ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye michuano hiyo iliyopangwa kufanyika Accra, Ghana.
Mashaga amewataka wadau wa ngumi za ridhaa kuendelea kuwaunga mkono ili wafanye vizuri kwani mabondia wote 11 waliopo kambini wanaendelea vizuri na wana ari kubwa ya kufanya vizuri kutokana na maandalizi wanayoendelea nayo kambini kwao Kibaha, Pwani.
Ngumi Ngumi waishukuru serikali
Ngumi waishukuru serikali
Read also
