Na mwandishi wetu
Matumaini ya timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kushiriki Michezo ya Olimpiki yameingia doa baada ya timu hiyo kulala kwa mabao 3-0 mbele ya timu ya taifa ya Afrika Kusini au Banyana Banyana.
Matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam yanaiweka Twiga katika wakati mgumu wa kupindua meza ikiwa ugenini timu hizo zitakaporudiana Jumatano ijayo.
Iwapo Twiga itafanikiwa kutoka na ushindi wa zaidi ya mabao matatu katika mechi hiyo ya marudiano itaumana na mshindi wa mechi ya Nigeria na Cameroon kabla ya kujua kama itafuzu kwenda Ufaransa kwenye Michezo ya Olimpiki baadaye mwaka huu.
Twiga katika mechi yake na Banyana ilizamishwa na mabao ya Thembi Kgatlana, Seoposenwe Jermaine na Hilda Magaia na kwa kipindi kirefu Banyana walionekana kuutawala mchezo dhidi ya Twiga waliokuwa wakishangiliwa na mashabiki wa nyumbani.
Kocha wa Twiga, Bakari Shime alikubali matokeo na kusema kwamba timu yake imefungwa na timu iliyo bora na kuongeza kuwa bao la kwanza walilopata wapinzani wao ni kama liliwavuruga na kujikuta wakikubali mabao mengine mawili.
Kimataifa Twiga Stars yalala 3-0 nyumbani
Twiga Stars yalala 3-0 nyumbani
Read also
