Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Alliance Girls FC, Ezekiel Chobanka amesema timu yake itajipanga upya kujiandaa na raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Wanawake ili ifanye vizuri zaidi.
Chobanka alisema hayo Jumatano hii akifafanua kuwa katika raundi ya kwanza timu yao haikufanya vizuri kutokana na uchanga wa kikosi hicho pamoja na kukosa uzoefu kwa wachezaji wao kwani wengi ni wapya.
“Kwa sasa ligi imesimama kwa muda kidogo, na sisi tumejipanga kuutumia muda huu wa mapumziko kikamilifu kujiandaa na michezo ya raundi ya pili.
“Tutacheza michezo kadhaa ya kirafiki ili kuipima timu kuelekea mechi zijazo za ligi tukiwa na imani ya kufanya vizuri zaidi kuliko kwenye mechi za mzunguko wa kwanza, hivyo mashabiki na wadau wajitokeze kwa wingi na tuwe pamoja kila mahali kutoa sapoti,” alisema Chobanka kocha wa zamani wa Mashujaa na The Tigers.
Katika msimamo wa ligi hiyo Alliance Girls ipo mkiani ikiwa na pointi tatu baada ya mechi tisa ilizocheza, imeshinda mechi moja na kupoteza nane huku ikifunga mabao manane na kufungwa 24.
Alliance Girls itacheza mchezo wake wa kwanza wa raundi ya pili Machi 13 dhidi ya Geita Queens katika Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.
Soka Alliance Girls kujipanga upya
Alliance Girls kujipanga upya
Related posts
Read also
