Na mwandishi wetu
Timu ya Singida Fountain Gate imeweka wazi kuwa itatumia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa michezo yote iliyosalia ya Ligi Kuu NBC.
Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza, alisema kuwa timu yao itatumia uwanja huo kwa kuwa uwanja wa nyumbani wa Liti, Singida unafanyiwa marekebisho.
“Hii ni kutokana na uwanja wa nyumbani CCM Liti uliopo Singida kuendelea kuwa chini ya matengenezo baada ya kufungiwa na Kamati ya Leseni ya TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kwa kutokidhi vigezo.
“Awali tulichagua uwanja wa Black Rhino uliopo mjini Karatu kuwa uwanja mbadala kwa mechi zetu za nyumbani, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu tumelazimika kubadili maamuzi,” alisema Massanza.
Alisema anawaomba wadau na mashabiki wa soka waliopo jijini Mwanza na viunga vyake kuwapokea na kuwaunga mkono kila watakaposhuka uwanjani kutafuta pointi tatu na kutimiza malengo yao waliyojiwekea msimu wa 2023-24.
Soka Singida FG wahamia CCM Kirumba
Singida FG wahamia CCM Kirumba
Read also
