Na mwandishi wetu
Kiungo mpya wa Simba, Edwin Balua amesema anaiona nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza licha ya ushindani mkubwa uliopo katika timu hiyo.
Mchezaji huyo alisema muda mfupi tangu ajiunge na miamba hiyo amebaini kiwango alichonacho anaweza kulishawishi benchi la ufundi chini ya kocha Abdelhak Benchikha na kumpa nafasi.
“Nafasi yangu ya kucheza kikosi cha kwanza Simba naiona, nipo tayari kwa mapambano na kufanya kila nitakachoelekezwa na makocha, sihofii ukubwa wa majina niliyoyakuta hapa sababu mpira siyo majina,” alisema Balua.
Kiungo huyo aliyetokea Tanzania Prisons, alisema anajua kucheza Simba kuna presha kubwa kutokana na mashabiki kuhitaji ushindi na kiwango bora, hivyo vyote amejipanga kuvikabili na anaamini atawafurahisha mashabiki zake.
Licha ya matumaini hayo lakini Balua anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa nyota wa kimataifa, Willy Onana na Saido Ntibazonkiza ambao ndio chaguo la kwanza la kocha Benchikha raia wa Algeria.
Soka Balua ajiona kikosi cha kwanza Simba
Balua ajiona kikosi cha kwanza Simba
Read also
