Riyadh, Saudi Arabia
Kipa wa zamani wa Man United ambaye kwa sasa hana timu, amekuwa akiwindwa na timu kadhaa za Ulaya na kwa sasa ya Al Shabab ya Saudi Arabia nayo imeingia katika mbio za kuisaka saini ya kipa huyo.
De Gea aliamua kuachana na Man United katika kipindi cha majira ya kiangazi msimu uliopita na hadi sasa ameendelea kuwa bila timu yoyote licha ya kuhusishwa na mipango ya kujiunga na timu kadhaa barani Ulaya.
Taarifa za chanzo kimoja cha habari zinadai kuwa, De Gea ambaye baada ya kuachana na Man United alijiweka kando na mpango wowote wa kwenda kucheza soka Saudi Arabia akiwa amepania kuendelea kucheza soka Ulaya, inadaiwa amefanya mazungumzo ya awali na mabosi wa Al Shabab.
De Gea amejiwekea heshima Man United kwa kuichezea timu hiyo kwa takriban miaka 12 akiwa ndiye kipa namba moja lakini alikataa mkataba mpya msimu uliopita na hadi sasa ameendelea kuwa mchezaji huru.
Baada ya kushindwa kumshawishi De Gea, kocha wa Man United, Erik ten Hag aliamua kumsajili Andre Onana kutoka klabu ya Inter Milan ya Italia na kwa sasa ndiye kipa namba moja wa timu hiyo.
Katika kinachoaminika kuwa ni mpango wa Al Shabab kujiimarisha, klabu hiyo pia inadaiwa kumtaka aliyekuwa kocha wa AS Roma, Jose Mourinho.
Kimataifa Al Shabab ya Saudia yamtaka De Gea
Al Shabab ya Saudia yamtaka De Gea
Read also
