Na mwandishi wetu
Beki wa kulia wa Simba SC, Shomari Kapombe ‘Baba Esther’ amesema bado ana misimu mitatu ya kuitumikia timu hiyo kabla ya kuanza kufikiria kustaafu kucheza soka.
Beki huyo wa kutumainiwa kwenye kikosi cha kocha Abdelhak Benchikha, alisema anaamini bado ana nguvu za kutosha pamoja na kiwango ambacho kinamruhusu kuitumikia timu hiyo.
“Bado nina uwezo wa kuhimili ushindani wa namba katika mashindano ya ndani na nje lakini kiwango changu bado kipo juu na sina majeraha ya mara kwa mara,” alisema Kapombe.
Mlinzi huyo alisema anatambua uongozi wa timu hiyo unasajili wachezaji wengi kutoka nje kutokana na malengo ya ushindani kwenye michuano ya kimataifa lakini yupo tayari kupigania namba yake hadi atakapostaafu.
Alisema anaamini bado ana kitu cha kuifanyia Simba, na kuirudisha kule ilipokuwa wakati walipobeba mataji manne ya Ligi Kuu NBC na kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kapombe ambaye kipaji chake kiliibukia akiwa timu ya vijana ya Simba, amekuwa mchezaji tegemeo na chaguo la kwanza la kila kocha aliyepita timu hiyo katika kipindi cha misimu sita tangu aliporejea Simba kwa mara ya pili akitokea Azam FC.
Soka Kapombe amebakisha misimu mitatu Simba
Kapombe amebakisha misimu mitatu Simba
Read also
