Barcelona, Hispania
Kocha wa Barca, coach Xavi Hernández anadaiwa kupitia kipindi kigumu akipambana kuwaweka kwenye mstari wachezaji wake baada ya timu hiyo kulala kwa mabao 4-1 mbele ya Real Madrid.
Jumapili iliyopita Barca ilichapwa mabao 4-1 na mahasimu wao Real Madrid katika mechi ya fainali ya Supercopa na habari za ndani zinadai kwamba tofauti zilizoibuka ndizo zilizochangia kipigo hicho.
Baadhi ya wachezaji wamekuwa wakihoji mwenendo wa timu na kuchukizwa na kauli ya Xavi kudai kwamba wachezaji wameshindwa kuendana na staili ya uchezaji ya Barca.
Habari zaidi zinadai kwamba si wachezaji wote wanaokubaliana na hoja ya Xavi hapo hapo kukiwa na wengine wanaodhani kwamba kocha huyo ameshindwa kuwa mkali kwa baadhi ya wachezaji kwenye kikosi hicho.
Watu waliokaribu na kocha huyo hata hivyo wanadai kwamba wachezaji wapo pamoja na kocha ingawa wanakiri kwamba si wote bali wako baadhi miongoni mwao wasioridhishwa naye.
Habari zilizotawala baada ya ushindi wa mabao 3-2 iliyoupata Barca dhidi ya Almeria siku chache kabla ya Krismasi zilidai kwamba ushindi huo ulitajwa kuwa mwanzo mzuri wa Barca kurudi katika ubora wake lakini kipigo mbele ya Real Madrid kimeibua hadithi mpya.
Xavi hata hivyo amewahi mara kadhaa kunukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba uhusiano baina yake na wachezaji wa timu hiyo haujawahi kuwa na matatizo yoyote.
Kimataifa Kipigo Barca chamtingisha Xavi
Kipigo Barca chamtingisha Xavi
Read also
