Na mwandishi wetu
Kocha wa Ihefu FC, Mecky Maxime amewataka wachezaji wake kutumia vipaji vyao kikamilifu kwa faida yao na kuipa matokeo mazuri timu hiyo.
Akizungumza na GreenSports, Maxime alisema nafasi waliyopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC haiendani na ukubwa wa majina na umaarufu waliokuwa nao katika ligi hiyo.
“Ligi ya msimu huu ni ngumu, inahitaji wachezaji wanaopambana na siyo umaarufu au ukubwa wa majina. Mimi na vijana wangu tunapaswa kupambana na kila mmoja kutimiza majukumu yake ili kuiondoa timu kwenye nafasi mbaya iliyopo hivi sasa,” alisema Maxime.
Alisema kuwa na wachezaji wazuri si kitu muhimu, kama wachezaji hao hawajitumi, hivyo atahakikisha anaandaa mpango mkakati utakaomwezesha kila mchezaji kuchangia mafanikio wanayakusudia.
Ihefu ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 13, imefanya usajili wa wachezaji; Elvis Rupia, Duke Abuya na Bruno Gomes wote kutoka Singida Fountain Gate kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kuelekea duru la pili la ligi hiyo.
Soka Maxime ataka vipaji vitumike Ihefu
Maxime ataka vipaji vitumike Ihefu
Read also
