Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Habib Kyombo ametamba kuwafunga waajiri wake wa zamani, Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi unaochezwa Jumatano hii kwenye dimba la Amaan, Zanzibar.
Akizungumza na GreenSports, mshambuliaji huyo alisema hiyo ni kutokana na kuwajua vyema mabeki wa timu hiyo pamoja na mtindo wa uchezaji wao.
“Mchezo utakuwa mgumu sababu ni nusu fainali lakini kwangu ni mchezo ambao nataka kuthibitisha uwezo wangu, najua haitokuwa rahisi sababu hata wao wanajua vizuri uchezaji wangu,” alisema Kyombo.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Singida msimu huu akitokea Simba, alisema anatambua hata mabeki wa Simba watakuwa wamemkamia lakini atatumia mbinu alizopewa na benchi lake la ufundi ili kutimiza ndoto zake.
Alisema si kwamba kuachwa na Simba ndio chanzo cha yeye kukamia bali ni kutaka kuipigania timu yake ipate ushindi na kubeba ubingwa wa taji hilo kwa mara ya kwanza.
Kyombo ndiye mfungaji wa bao la ushindi lililoipeleka Singida nusu fainali walipoizamisha Azam mabao 2-1 Jumatatu iliyopita.
Soka Kyombo apania kuifunga Simba
Kyombo apania kuifunga Simba
Read also
