Eldoret, Kenya
Watu wawili wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na mauaji ya mwanariadha wa Uganda, Benjamin Kiplagat aliyeuawa mjini Eldoret, Kenya na mwili kukutwa ndani ya gari lake ukiwa na majeraha.
Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Moiben, Stephen Okal alisema kwamba kisu kinachodaiwa kutumika kumuua Kiplagat kilikutwa kwa mmoja wa watuhumiwa.
Mauji ya Kiplagat, 34, kwa mujibu wa Kamanda Okal chanzo chake kinadhaniwa kuwa ni wizi uliokusudiwa kufanywa na watuhumiwa kwa kuwa simu na fedha za marehemu vyote vilichukuliwa.
Kiplagat aliiwakilisha Uganda katika Michezo ya Olimpiki mara tatu na kwenye mashindano ya dunia ya riadha aliiwakilisha nchi hiyo mara sita akishiriki mbio za mita 3,000 na katika mashindano ya Afrika mwaka 2012 alishinda medali ya shaba.
Mauaji ya Kiplagat yanakuwa ni tukio la nne kutokea kwa mwanaridha wa nchini Kenya kwa miaka ya hivi karibuni.
Mwaka 2021, bingwa mara mbili wa mashindano ya dunia ya Mbio za Nyika, Agnes Tirop aliuawa katika mji wa kwao wa Iten, mume wake hadi sasa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji.
Mwanariadha mzaliwa wa Kenya aliyeiwakilisha Bahrain, Damaris Muthee, mwili wake ulikutwa katika nyumba ya mwanariadha mwenzake, tukio ambalo lilitokea mwaka 2022.
Katika tukio jingine mwanariadha, Rubeyita Siragi aliuawa mwezi Agosti katika tukio ambalo polisi nchini Kenya walilihusisha na ugomvi wa kugombea mwanamke.
Riadha Wawili wakamatwa mauaji ya mwanariadha
Wawili wakamatwa mauaji ya mwanariadha
Read also
