Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Adel Amrouche, amemrejesha kwenye kikosi chake beki Mohamed Hussein Zimbwe Jr katika kikosi cha awali cha maandalizi ya fainali za Afcon 2024.
Zimbwe Jr ambaye pia ni beki wa timu ya Simba, mara ya mwisho kuitwa timu ya taifa ilikuwa Machi 26, mwaka huu wakati wa michezo ya kutafuta nafasi ya kufuzu fainali za Afcon 2024 dhidi ya Uganda.
Amrouche amewaita kwa mara ya kwanza Cyprian Kachwele (Vancouver White Caps), Omary Mvungi (Nantes), Zion Nditi (Aldershot Town), Adolf Bitegeko (Volsungur IF), Tarryn Allarakhia (Wealdstone FC) , Miano Danilo (Telford United) , Twariq Ahmed (Telford United) , Mark John (Kingston FC) .
Wengine ni Mohamed Ali (Boreham Wood), Roberto Nditi (Forfar Athletic), Ayoub Bilali (FK Gorazde), Pellegrino Ahmal (Bodo), Adam Kasa (IFK Haninge) na Said Khamis (FK Jedinstvo) wanaocheza kwenye klabu mbalimbali barani Ulaya.
Kocha huyo pia amemuita kwa mara ya kwanza winga Edwin Balua anayekipiga kwenye klabu ya Tanzania Prisons ya Mbeya.
Wachezaji wengine wanaounda kikosi hicho ni makipa Aishi Manula, Beno Kakolanya, Abutwalib Mshery, Metacha Mnata.
Mabeki ni Dickson Job, Ibrahim Bacca, Bakar Mwamnyeto, Lusajo Mwaikenda, Nickson Kibabage, Haji Mnoga , Abdi Banda, , AbdulMaik Zakaria, Isarel Mwenda na Mohamed Hussein.
Viungo ni Omar Mvungi, Mzamiru Yasin, Yusuph Kagoma, Sospeter Bajana, Baraka Majogoro, Feisal Salum, Mudathir Yahya, Morice Abraham, Himid Mao.
Washambuliaji ni Ladaki Chasambi, Mbwana Samata, Saimon Msuva, Kibu Denis, Abdul Suleiman, Ben Starkie, Matheo Anton, Charles Mmombwa, Joshua Ibrahim, Clement Mzize, Kennedy Juma, Khlefin Hamdoun na Adam Salamba.
Kimataifa Amrouche amrejesha Zimbwe Jr Stars
Amrouche amrejesha Zimbwe Jr Stars
Read also
