Manchester, England
Kauli aliyowahi kuitoa kocha wa Man City, Pep Guardiola kwamba timu yake ina uwezo wa kulitetea taji la Ligi Kuu England imeanza kuibua maswali kutokana na mwenendo usiovutia wa timu hiyo.
Mbio za Man City kulitetea taji hilo zimeendelea kukumbana na dhoruba baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Crystal Palace, katika mechi ya EPL iliyopigwa jana Jumamosi.
Katika mechi hiyo ambayo Man City ilikuwa nyumbani, timu hiyo ilifanikiwa kuongoza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Jack Grealish dakika ya 24 na Rico Lewis dakika 10 baada ya mapumziko.
Palace hata hivyo walifanikiwa kuokoa bao la kwanza dakika ya 76 lililofungwa na Jean-Philippe Mateta kabla ya kumalizia bao la pili lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Michael Olise.
Penalti hiyo ilitolewa katika dakika tano za nyongeza baada ya Phil Foden kumchezea ndivyo sivyo Mateta na hivyo kutosha kuibua maswali juu ya mwenendo wa Man City na ubora wao katika EPL.
Kilichowashangaza wengi katika mechi na Palace ni jinsi timu hiyo ilivyoweza kutawala vyema mchezo na kufanikiwa kuifungua na kuipenya safu ngumu ya ulinzi ya Palace iliyojipanga vyema lakini baadaye mambo yakaanza kuwaharibikiwa.
Matokeo hayo yanakuwa ni sare ya tatu kwa Man City kuipata kwenye uwanja wake wa nyumbani na sasa mabingwa hao watetezi wanashika nafasi ya nne wakiwa nyuma ya Liverpool kwa tofauti na pointi tatu na Liverpool leo Jumapili wapo uwanjani dhidi ya Man United.
Matokeo ya mechi za EPL jana Jumamosi…
Chelsea 2-0 Sheff Utd
Man City 2-2 Crystal Palace
Newcastle 3-0 Fulham
Burnley 0-2 Everton
Kimataifa Kasi ya Man City EPL yaibua maswali
Kasi ya Man City EPL yaibua maswali
Read also
