Na mwandishi wetu
Simba leo Ijumaa imeichapa Kagera Sugar mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huo ukiwa ushindi wa kwanza wa kocha wao mpya, Abdel hak Benchikha.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 22 katika ligi hiyo ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga yenye pointi 24 ambayo kesho itaumana na Mtibwa Sugar katika mwendelezo wa ligi hiyo ambayo usukani wake unashikiliwa na Azam FC.
Simba iliandika bao la kwanza katika kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliojazwa wavuni na Saido Ntibazonkiza ambaye alilazimika kupiga penalti hiyo mara ya pili baada ya kipa wa Kagera kutoka katika eneo lake mapema na mwamuzi kuamuru penalti irudiwe.
Mabao mengine mawili ya Simba yalipatikana kipindi cha pili wafungaji wakiwa ni Sadio Kanoute na mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo, John Bocco.
Benchikha baada ya mechi hiyo aliwasifia wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kutengeneza nafasi za kufunga ingawa alikiri kwamba wanahitaji kufanyia kazi umaliziaji wa nafasi wanazotengeneza.
Soka Simba yaiadhibu Kagera Sugar
Simba yaiadhibu Kagera Sugar
Read also
