London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekwepa adhabu ambayo angepewa na Chama cha Soka England (FA) kwa kauli yake ya kulaumu matumizi ya VAR katika mechi na Newcastle ambayo Arsenal ililala kwa bao 1-0.
Newcastle ilipewa bao hilo pekee na la ushindi baada ya kuangaliwa kwa picha za VAR jambo ambalo lilimekra Arteta na kusema kwamba uamuzi huo ni fedheha na aibu katika Ligi Kuu England (EPL).
Baadaye taarifa ya FA ilitolewa ikidai kumkuta na hatia kocha huyo kwa kutoa kauli isiyofaa na kumpa siku za kujitetea kabla ya kutangazwa kwa adhabu ambayo angepewa.
FA hata hivyo katika taarifa yake iliyopatikana jana Alhamisi ilieleza kuwa, kamati huru ya uchunguzi imeona hakuna ushahidi wa jambo lolote baya baada ya kusikiliza suala hilo.
“Ilidaiwa kwamba kauli aliyoitoa ilikwenda kinyume na maadili kwa maana ya kwamba kulikuwa na kauli za kudhalilisha waamuzi na au kushusha hadhi ya mchezo wa soka na kuuweka katika hali ya hatari,” ilieleza taarifa ya FA.
Taarifa ya kufuta kusudio la kumuadhibu Arteta ilieleza kwamba kocha huyo alitumia neno ‘disgrace’ (fedheha-aibu) ambalo kwa lugha ya Kihispaniola anayozungumza kocha huyo neno hilo hilo linaweza kufanana katika matamshi na kutafsiriwa kwa maana ya ‘bahati mbaya’ au janga.
Taarifa hiyo pia ilifafanua kuwa wakati kwa lugha ya kiingereza neno hilo hilo linaweza kutafsiriwa kuwa ni la kudhalilisha au kukosea mtu heshima lakini kwa mtamkaji inaweza kuwa si maana iliyokusudiwa.
Kimataifa FA yamsafisha Arteta
FA yamsafisha Arteta
Read also
