London, England
Ndoto za Newcastle kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya zimeota mbawa baada kuishia hatua ya makundi ikilala kwa mabao 2-1 mbele ya AC Milan jana Jumatano ingawa mashabiki wake wanaamini huo si mwisho wa ndoto zao.
Mashabiki hao wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani St Jame’s Park waliinua juu bendera yenye maandishi yaliyositiza kuwa kilichowakuta hakimaanishi kwamba huo ndio mwisho wa ndoto zao.
Kwa kipigo hicho maana yake ni kwamba Newcastle inashika mkia Kundi F na kama ilivyo Man United nayo inakosa nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora pamoja na kukosa nafasi kushiriki michuano ya Europa Ligi.
Timu nyingine zilizotolewa kama Newcastle na Man United na kupoteza yote Ulaya ni Sevilla, Union Berlin, Benfica na Royal Antwerp,
England inabaki na wawakilishi wawili katika hatua ya mtoano au 16 bora ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Man City na Arsenal, wote wanasubiri droo ya ligi hiyo itakayofanyika Desemba 18 mjini Nyon, Switzerland ili kila timu kumjua mpinzani wake.
Timu nyingine ambazo zimefuzu zipo katika makundi mawili ambayo katika droo hiyo yatazingatiwa kwa kila timu kumjua mpinzani wake…
Kundi la kwanza: Barcelona, Borussia Dortmund, Arsenal, Atletico Madrid, Man City, Real Madrid, Real Sociedad na Bayern Munich.
Kundi la pili: Lazio, Napoli, PSV Eindhoven, Paris Saint Germain, FC Porto, Copenhagen, Inter Milan na RB Leipzig, Celtic, Red Star Belgrade,
Kimataifa Newcastle yakwama Ulaya
Newcastle yakwama Ulaya
Read also
