Ujerumani
Wenyeji wa fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 24, Ujerumani wataanza mechi ya ufunguzi kwa kuumana na Scotland baada ya droo ya makundi ya fainali hizo kutangazwa Jumamosi hii na timu hizo kupangwa Kundi A.
Mechi ya ufunguzi wa fainali hizo itapigwa Ijumaa ya Juni 14 kwenye dimba la Allianz Arena mjini Munich wakati England itacheza mechi yake ya kwanza Juni 16 dhidi ya Serbia.
Timu nyingine zilizo katika Kundi A ni Hungary na Switzerland wakati England imepangwa Kundi C ambalo pia lina timu za Denmark pamoja na Slovenia.
Mabingwa watetezi wa fainali hizo, Italia wao wamepangwa Kundi B pamoja na timu za Hispania, Croatia na Albania na mechi ya fainali itakayomtangaza bingwa mpya wa michuano hiyo itapigwa Julai 14 kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.
Makundi ya fainali hizo ni kama ifuatavyo…
Kundi A: Ujerumani, Scotland, Hungary na Switzerland
Kundi B: Hispania, Croatia, Italia na Albania
Kund C Slovenia, Denmark, Serbia na England
Kundi D Uholanzi, Austria, Ufaransa na (mshindi play-off-A)
Kundi E: Ubelgiji, Slovakia, Romania na (mshindi play-off-B)
Kundi F: Uturuki, Ureno, Jamhuri ya Czech (mshindi play-off-C)
Play off A-Poland, Estonia, Wales, Finland, Estonia
Play off B- Israel, Bosnia-Herzegovina, Ukraine, Iceland
Play off C- Georgia, Ugiriki, Kazakhstan, Luxembourg
Kimataifa Ujerumani, Scotland kufungua pazia Euro 24
Ujerumani, Scotland kufungua pazia Euro 24
Read also
