London, England
Tottenham Hotspurs inajiandaa kujiimarisha kwa usajili wakati wa dirisha dogo la Januari lengo likiwa ni kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo ambayo inaonekana kuanza kupoteza makali.
Kocha wa Spurs, Ange Postecoglou (pichani) amesema timu yake kwa sasa inaandamwa na wachezaji majeruhi akiwamo Rodrigo Bentancur ambaye hivi karibuni aliongeza idadi ya majeruhi katika timu hiyo.
Januari mwakani timu hiyo inaweza kujikuta pabaya zaidi kwa kuwakosa nyota wake ambao watakuwa wakiziwakilisha timu zao za taifa kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast.
Spurs iliuanza msimu huu vizuri na kuanza kutajwa kutoa upinzani katika mbio za kulibeba taji la Ligi Kuu England (EPL) baada ya kushika usukani kabla ya kuanza kupotea njia kutokana na vipigo katika mechi za hivi karibuni.
Timu hiyo ilijikuta pagumu baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 mbele ya Chelsea lakini pia ikalala kwa mabao 2-1 mbele ya Wolverhampton Wanderers kabla ya Aston Villa nao kuwachapa 2-1.
Matokeo hayo yameibua hofu na sasa kocha Postecoglou anaamini upo umuhimu wa kukiimarisha kikosi chake kabla mambo hayajaendelea kuwa mabaya.
Kwa sasa Spurs inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza mechi 13 na Jumapili kesho itakuwa na kibarua kigumu kwenye dimba la Etihad dhidi ya Man City, mabingwa watetezi EPL.
Kimataifa Kocha Spurs ajiandaa kusajili Januari
Kocha Spurs ajiandaa kusajili Januari
Read also
