Na mwandishi wetu
Wachezaji Pacome Zouzoua, Khalid Aucho na Clement Mzize wameingia katika kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Yanga kwa Mwezi Novemba.
Nyota hao wameingia kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo katika mechi walizocheza za mwezi huo.
Huo ni utaratibu ambao klabu hiyo imejiwekea tangu kuanza kwa msimu huu ukiwa na lengo la kuongeza hamasa kwa wachezaji wake kujituma na kuipa mafanikio timu katika mashindano yote wanayoshiriki.
Mbali na tuzo hiyo pia mchezaji hujinyakulia kitita cha Sh milioni 4 taslimu na zawadi nyingine kutoka kwa wadhamini wa tuzo hiyo, Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Kiungo wa Burkinafaso, Stephen Aziz Ki, ndiye mchezaji wa kwanza kuibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa mwezi uliopita baada ya kuwashinda wachezaji wenzake, Maxi Nzengeli na beki Dickson Job.
Soka Aucho, Pacome, Mzize wawania tuzo ya mwezi
Aucho, Pacome, Mzize wawania tuzo ya mwezi
Read also
