Riyadh, Saudi Arabia
Cristiano Ronaldo amefanya kitu kinachoweza kuonekana cha ajabu kwa kukataa penalti aliyopewa na mwamuzi wakati Al-Nassr ikiumana na Persepolis ya Iran katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Asia.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 38 alichukua uamuzi huo katika mechi iliyopigwa Jumatatu usiku na katika dakika ya pili tu ya mchezo huo, aliangushwa na mwamuzi aliashiria ipigwe penalti lakini Ronaldo akamshawishi mwamuzi kwamba haikuwa penalti.
Mwamuzi wa mechi hiyo, Ma Ning kutoka China baadaye aliliangalia tukio hilo kwa uhakika na kukubaliana na Ronaldo kwa uamuzi wa kuifuta penalti hiyo.
Uamuzi huo wa kutumia VAR pamoja na ushawishi wa Ronaldo viliiokoa timu ya Persepolis ambayo hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa 0-0 licha ya Al Nassr kupata pigo kwa kucheza 10 uwajani baada ya Ali Lajani kupewa kadi nyekundu dakika ya 17.
Al Nassr hata hivyo tayari imefuzu hatua ya mtoano ya ligi hiyo kabla ya hata ya mechi na Persepolis ikiwa ndiye kinara wa Kundi E baada ya kukusanya pointi 13 katika mechi tano wakati Persepolis inashika nafasi ya pili.
Kimataifa Ronaldo apewa penalti, aikataa
Ronaldo apewa penalti, aikataa
Read also
