Na Joseph Shaluwa
Msanii nyota wa Afropop, Mr Eazi, ameachia albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘The Evil Genius’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.
Video za albamu hiyo imechukuliwa katika maeneo ya miji ya nchi tofauti kama, Ouidah na Cotonou nchini Benin, Kigali, Rwanda, Accra na Kokrobite, Ghana, Lagos, Nigeria, London, Uingereza na Los Angeles na New York, Marekani.
Albamu hiyo ‘The Evil Genius’ huangazia baadhi ya kazi za kibinafsi za Mr Eazi, anapozama kwa kina katika mada kama vile mapenzi, usaliti, upweke na familia, zinazoonyeshwa kupitia vitendo vitatu tofauti.
Washiriki katika kazi hiyo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni Angelique Kidjo (Benin), Tekno (Nigeria), Efya (Ghana), Whoisakin (Nigeria), Joeboy (Nigeria), na washindi mara tatu wa Grammy Soweto Gospel Choir (Afrika Kusini).
Kwa upande wa watayarishaji, walikuwa pamoja na Kel-P (Nigeria), Knucks (U.K.), Michael Brun (Haiti), Andre Vibez (Nigeria), Yung Willis (Nigeria), Nonso Amadi (Nigeria/Canada), KillBeatz (Ghana), M.O.G Beatz (Ghana), E Kelly (Nigeria), Type A (Nigeria), Stikmatik (U.K.), Phantom (Nigeria), Beat Butcha (U.K.), Venna (U.K.), KDream (Nigeria) na Mr Eazi mwenyewe.
Katika kuonyesha Mr Eazi ni mwamba wa kuchanganya ladha, ndani yake yupo staa kutoka Afrika Mashariki nchini Kenya, Alphonce Odhiambo maarufu Alpha ODH ambaye amemshirikisha kwenye kibao ‘Advice’.
Kwa upande wa usanifu wa jalada la albamu hiyo, Mr Eazi alishirikiana na mwanamitindo maarufu wa Nigeria, mbunifu na mpiga picha Daniel Obasi, anayejulikana kwa kazi nzuri alizowafanyia mastaa Beyoncé na Louis Vuitton.
Burudani Mr Eazi akamilisha ‘Evil Genius’
Mr Eazi akamilisha ‘Evil Genius’
Related posts
Read also
