London, England
Kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham na beki wa Chelsea, Levi Colwill wamejitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kinachojiandaa kwa mechi dhidi ya Malta na Macedonia kila mmoja akiwa na tatizo la bega.
Kujitoa kwa wachezaji hao kunafanya idadi ya wachezaji wa kikosi hicho watakaokosekana katika mechi hizo za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 24 kuwa watano baada ya awali, James Maddison, Callum Wilson na Lewis Dunk nao kulazimika kujitoa kwa kuwa majeruhi.
Wachezaji wengine wa timu hiyo, mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford na kiungo wa Man City, Kalvin Phillips watachelewa kuungana na wachezaji wenzao kutokana na sababu mbalimbali binafsi.
England chini ya kocha Gareth Southgate tayari imefuzu fainali hizo na iwapo itapata ushindi mmoja katika mechi yake ya Kundi C hapo itakuwa imejihakikishia kushika usukani wa kundi hilo.
Timu hiyo itacheza mechi hizo mbili zitakazopigwa Novemba 17 na 20 na baada ya hapo itajikita katika maandalizi ya fainali hizo ambazo zitafanyika Juni mwakani nchini Ujerumani.
Kimataifa Bellingham ajiweka kando England
Bellingham ajiweka kando England
Read also
