Dortmund, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane anazidi kuuwasha moto kwenye Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga baada ya kufunga mabao matatu (hat trick) Bayern ikiichapa Borussia Dortmund 4-0.
Hiyo inakuwa hat trick ya tatu kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenham na hivyo kuiweka pazuri Bayern inayosaka taji la 12 mfululizo la Bundesliga ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kane pia anakuwa ameifungia Bayern mabao 15 katika ligi hiyo lakini pia anakuwa amefikisha jumla ya mabao 19 msimu huu kwa Bayern pamoja na timu yake ya taifa ya England.
Mabao hayo pia yanamfanya awe mchezaji wa kwanza kufunga mabao 15 katika mechi 10 za kwanza za Bundesliga na sasa ndiye anayeshika usukani kwa wafungaji wenye mabao mengi kwenye ligi hiyo.
Kwa Dortmund matokeo hayo ya jana Jumamosi yanakuwa yameivunja rasmi rekodi waliyokuwa wakijivunia ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi hiyo tangu Aprili Mosi
Mabao ya washindi yalipatikana kuanzia dakika ya nne, la kwanza likifungwa na Dayot Upamecano kabla Kane hajaisambaratisha Dortmund kwa mabao ya dakika za 3, 72 na 90.
Bayern katika mechi hiyo ilipata pigo baada ya kocha wake Thomas Tuchel kulimwa kadi dakika ya 43 baada ya kuonekana akiwakoromea waamuzi.
Matokeo ya mechi za Bundesliga Jumamosi hii ni kama ifuatavyo…
B Dortmund 0-4 Bayern Munich
Köln 1-1 Augsburg
Union Berlin 0-3 Frankfurt
Mainz 2-0 RB Leipzig
Freiburg 3-3 B Mgladbach
Hoffenheim 2-3 B Leverkusen
Kimataifa Kane apiga hat trick ya tatu Bundesliga
Kane apiga hat trick ya tatu Bundesliga
Read also
