Cairo, Misri
Baada ya mgogoro wa muda mrefuh hatimaye FIFA imeziondoa, Kenya na Zimbabwe katika mbio za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023.
Uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya nchi hizo kukwama katika mbio zao za kuwania kufutiwa adhabu na FIFA katika muda uliowekwa ambao ni wiki hii.
Vyama vinavyosimamia soka katika nchi za Kenya na Zimbabwe vilisimamishwa uanachama wa FIFA Februari mwaka huu na hivyo kutoruhusiwa kushiriki katika mashindano ya soka yanayotambuliwa na FIFA kwa kilichoelezwa kuwa ni viongozi wa kisiasa wa nchi hizo kuingilia mambo ya soka.
Taarifa ya CAF iliyopatikana hii leo ilieleza, “Vyama viwili vya Football Kenya Federation-FKF (Shirikisho la Soka Kenya) na Zimbabwe Football Association-ZFA (Chama cha Soka Zimbabwe) wanachukuliwa kama walioshindwa na wanaondolewa katika mashindano.”
Kwa uamuzi huo wa CAF maana yake ni kwamba Kundi C litakuwa na timu tatu kama itakavyokuwa kwa Kundi K na utaratibu wa mechi zao utakuwa kama ulivyopangwa. Katika mbio za kuwania kufuzu, timu mbili za kwanza katika kila kundi ndizo zitakazofuzu fainali hizo zilizopangwa kufanyika kati ya Juni na Julai mwakani nchini Ivory Coast.
Kenya ilipangwa Kundi C na timu za Cameroon, Namibia na Burundi na walitarajia kutupa karata yao ya kwanza Juni 4 dhidi ya Cameroon mjini Yaounde wakati Zimbabwe ilikuwa na Morocco, Afrika Kusini na Liberia na mechi yao ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Morocco.
Nchini Kenya serikali ya nchi hiyo ilimuondoa madarakani rais wa KFF, Nick Mwendwa kwa tuhuma za rushwa wakati nchini Zimbabwe serikali ya nchi hiyo iliivunja kamati ya utendaji ya ZFA kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
Mwendwa alifika mahakamani mara kadhaa kwa ajili ya mashitaka yaliyokuwa yakimkabili lakini baadaye alishinda kesi hiyo na kufutiwa mashitaka baada ya kukosekana ushahidi dhidi yake.
Kimataifa Kenya yafutwa rasmi AFCON 2023
Kenya yafutwa rasmi AFCON 2023
Related posts
Read also
