Na mwandishi wetu
Tanzania imepanda nafasi moja kutoka nafasi ya 122 hadi ya 121 kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa mwezi Oktoba vilivyotolewa leo Alhamisi.
Huenda kufanya vizuri kwa timu ya taifa kumeipa nafasi hiyo, kwani ilitoka kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Sudan hivi karibuni katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa nchini Saudi Arabia.
Pia, Tanzania ni miongoni mwa mataifa 24 yaliyofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika nchini Ivory Coast, mwakani.
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni ya 65, Uganda licha ya kutofuzu Afcon inashika nafasi ya 90 ikishuka nafasi moja, ikifuatiwa na Kenya ya 110, Sudan ni ya 130, Rwanda ya 140 na Burundi ya 142.
Ethiopia ya 143 wakati Sudan Kusini ni ya 167, Djibouti imepanda nafasi moja mpaka 189 na Somalia ikishuka nafasi mbili ikidondokea nafasi ya 196.
Kwa Afrika kinara ni Morocco ambayo ni ya 13 duniani, Senegal ya 20, Tunisia imeshuka nafasi tatu na kuangukia ya 32, Algeria ya 33, Misri ya 35, Nigeria ya 40, Cameroon ya 43 na Mali imeshika nafasi ya 47.
Kidunia, Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ufaransa, Brazil, England, Ubelgiji, Ureno, Uholanzi, Hispania, Italia na Croatia.
Kimataifa Tanzania yapanda Fifa
Tanzania yapanda Fifa
Read also
