London, England
Kocha wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou (pichani) ameweka historia kwa kutwaa kwa mara ya pili tuzo ya kocha bora wa mwezi na kuwa kocha wa kwanza katika Ligi Kuu England kubeba tuzo hiyo katika miezi yake miwili ya kwanza.
Postecoglou, 58, kocha kutoka Australia ameiongoza vyema Spurs na kuipaisha juu katika msimamo wa EPL akiwa na rekodi ya kutopoteza hata mechi moja kati ya nane, akishinda sita na kutoka sare mara mbili.
Kocha wa mwisho kubeba tuzo hiyo mara mbili mfululizo ni Jurgen Klopp wa Liverpool ambaye alifanya hivyo msimu wa 2019-20, msimu ambao Livepool pia ilibeba taji la EPL.
Huu ni msimu wa kwanza kwa Postecoglou na Spurs ambapo alikabidhiwa jukumu hilo kutoka kwa kocha Mtaliano, Antonio Conte ambaye aliingia katika mzozo na wamiliki wa klabu hiyo kabla ya kujikuta akilazimika kuachia ngazi.
Mambo hata yanaonekana kuwa mazuri kwa Spurs msimu huu kwani mbali na Postecoglou, nahodha wa timu hiyo, Son Heung-min alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba.
Kimataifa Kocha Spurs abeba tuzo ya mwezi
Kocha Spurs abeba tuzo ya mwezi
Read also
