London, England
Winga wa Arsenal, Bukayo Saka ameachwa katika kikosi cha England kinachojiandaa na mechi dhidi ya Australia na Italia kwa sababu ya kuwa majeruhi.
Saka ambaye anasumbuliwa na matatizo ya misuli, aliikosa mechi ya juzi Jumapili ya Ligi Kuu England dhidi ya Man City ambayo Arsenal ilishinda kwa bao 1-0.
Taarifa ya FA imethibitisha hilo ikieleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya timu ya madaktari wa England kumfanyia vipimo mchezaji huyo na kuongeza kwamba nafasi yake hatopewa mchezaji mwingine wakati huu kikosi cha England kikiwa na wachezaji 25.
Timu ya England inajiandaa kuuma na Australia Oktoba 13 na siku nne baadaye itaumana na Italia katika mechi za kuwania kufuzu Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alisema baada ya mechi na Man City kwamba mchezaji huyo hawezi kuwamo kwenye kikosi cha England na kwamba hakufanya mazoezi hata simu moja tangu aumie.
Arteta hata hivyo hakuweka wazi ni lini hasa mchezaji huyo atakuwa fiti badala yake aliishia kusema kwamba kwa wakati huu hawezi kucheza soka.
Baada ya kukosa mechi na Man City, Saka anabaki na rekodi ya kucheza mfululizo mechi 87 za Ligi Kuu England akiwa na timu ya Arsenal.
Kimataifa Saka aachwa England
Saka aachwa England
Read also
