Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski yumo katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa kwenda kucheza soka katika ligi ya Saudi Arabia.
Saudi Arabia ipo katika mkakati mzito wa kuiboresha ligi yao pamoja na soka la nchini humo kwa kusajili kwa pesa nyingi wanasoka mastaa wanaotamba hasa barani Ulaya na chanzo kimoja cha habaru kimedokeza kuwa mchezaji huyo naye anawindwa Saudi Arabia.
Chanzo hicho hata hivyo haikuweka wazi jina la klabu inayomuwinda mshambuliaji huyo lakini inaeleweka kwamba ni moja ya klabu mbili mahasimu katika jiji la Riyadh za Al Nassr ni Al Hilal.
Lewandowski mwenye miaka 35 sasa, alijiunga na Barca Julai mwaka jana akitokea Bayern Munich, klabu ambayo kwa kiasi kikubwa imebeba historia ya mafanikio yake kwenye soka barani Ulaya.
Akiwa Bayern, Lewandowski aliweka rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao 344 katika mechi 375 na kutwaa mataji na tuzo mbalimbali zikiwamo za mfungaji bora kwa miaka minane.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Poland, licha ya mafanikio hayo, aliamua kuondoka Bayern na kwenda Barca kwa alichodai kwamba anataka changamoto mpya na sasa swali linabaki je atakuwa tayari kwa changamoto nyingine mpya ya Saudi Arabia.
Miongoni mwa wachezaji mastaa wa Ulaya ambao wametimkia Saudi Arabia ni Cristiano Ronaldo, Neymar, N’Golo Kante, Eduardo Mendy, Karim Benzema na wengineo.
Kimataifa Lewandowski atakiwa Saudi Arabia
Lewandowski atakiwa Saudi Arabia
Read also
