Na mwandishi wetu
Straika mpya wa Singida Fountain Gate, Elvis Rupia ameanza vyema kuiwakilisha timu hiyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufunga bao pekee na la ushindi kwa timu hiyo dhidi ya Future ya Misri.
Straika huyo aliyesajiliwa kutoka AFC Leopards ya Kenya hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza na Singida katika michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa katika michuano ya klabu barani Afrika.
Singida imeumana na Future Jumapili hii kwenye Uwanja wa Azam Complex katika mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo, ilipata bao hilo na kulilinda vyema kwa dakika zote 90 za mchezo huo.
Matokeo hayo yanakuwa mwanzo mzuri kwa timu hiyo ingawa sasa itakuwa na kibarua cha kulinda ushindi huo timu hizo zitakaporudiana baadaye mwezi huu ili kujihakikishia tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.
Misri ni taifa linalosifika kwa soka barani Afrika hivyo ushindi mwembamba hautoshi kuifanya Singida ijiaminishe kuwa tayari imefuzu michuano hiyo.
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya klabu barani Afrika ni timu za Yanga na Simba ambazo zinashiriki Ligi ya Mabingwa, Yanga katika mechi ya kwanza imetoka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Al-Merreikh ya Sudan wakati Simba ilitoka sare ya mabao 2-2 ugenini mbele ya Power Dynamos ya Zambia.
Kimataifa Straika mpya Singida aanza vizuri
Straika mpya Singida aanza vizuri
Read also
