Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Bernard Morrison amepewa jezi namba tano katika timu yake mpya ya AS FAR ya Morocco.
Morrison ameweka wazi juu ya hilo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa na jezi hiyo akionesha kufurahishwa na uteuzi wa namba ya jezi hiyo.
Taarifa mbalimbali zimefafanua kuwa Morisson amepewa mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo inayonolewa na kocha Nasreddine Nabi anayeelezwa kumuhitaji mchezaji huyo wa Ghana baada ya kufanya naye kazi Yanga kabla ya wote kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
Awali, Morrison aliyeondoka Yanga akiwa huru baada ya kumaliza mkataba wake alikuwa akionekana akifanya mazoezi na sehemu ya kikosi hicho kabla ya hivi karibuni kuelezwa amekamilisha dili lake hilo.
Mbali na Yanga, Morrison pia aliwahi kuitumikia Simba kwa nyakati mbili tofauti pia amewahi kukipiga DC Motema Pembe na AS Vita za DR Congo, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na sasa anaanza maisha mapya Afrika ya Kaskazini.
Kimataifa Morrison apewa jezi namba 5
Morrison apewa jezi namba 5
Read also
