Na mwandishi wetu
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo (pichani) anatarajia kupanda ulingoni kupambana na Mkenya, Rayton Okwiri kwenye pambano la kuwania mkanda wa ubingwa wa IBA.
Ali Mndeme ambaye ni promota wa pambano hilo, ameeleza kuwa mabondia hao watapambana Septemba 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Mndeme alisema kwamba pambano hilo litakuwa la uzito wa kati na kwamba mipango yote ya maandalizi kuelekea pambano hilo inakwenda vizuri.
“Kila kitu kinakwenda vizuri, tunatarajia kuwa na pambano lenye hadhi ya kimataifa, ukiachilia mbali mechi ya kina Mwakinyo lakini pia kila bondia atakayepanda ulingoni kwenye mapambano ya utangulizi, ataonesha ubora wake wa hali ya juu,” alisema Mndeme.
Akimzungumzia zaidi Mwakinyo alisema kwamba anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya pambano hilo akiwa na kiu kubwa ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania siku hiyo dhidi ya mpinzani.
Pambano la Mwakinyo na Okwiri limekuja ikiwa ni takriban miaka miwili imepita tangu bondia huyo kutoka Kenya kudai kwamba anahitaji pambano na Mwakinyo.
Ngumi Mwakinyo, Okwiri ulingoni
Mwakinyo, Okwiri ulingoni
Read also
