Na mwandishi wetu
Waamuzi wa soka Tanzania, Kassim Mpanga, Nassir Salum, Ahmed Arajiga (pichani) na Frank Komba, wameteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa waamuzi wa mechi za kuwania kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (CAF) iliyopatikana Jumatano hii ilieleza kuwa waamuzi hao watachezesha mechi kati ya FC Lupopo ya DR Congo itakayoumana na Sekhukhune United ya Afrika Kusini, itakayopigwa Septemba 16 mwaka huu.
Katika soka la wanawake waamuzi wengine wa Tanzania, Tatu Malogo na Glory Tesha wameteuliwa kuwa waamuzi wa mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Wanawake Afrika (AWC 2024) kati ya Uganda na Algeria itakayopigwa Septemba 20 mwaka huu.
Wakati huo huo viongozi wawili wa soka nchini, Somoe Ng’itu ambaye ni kaimu mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania na Khalid Abdallah ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF nao wameteuliwa na CAF kuwa wasimamizi wa mechi za michuano ya Afrika.
Ng’itu ameteuliwa kuwa kamisaa wa mechi ya kufuzu mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC-2024) kati ya Ethiopia na Burundi itakayochezwa Septemba 26 mwaka huu wakati Abdallah yeye ameteuliwa kuwa kamishna wa mechi ya Kombe la Shirikisho (CAFCC) kati ya Arta Solar ya Djibouti na Zamalek ya Misri itakayopigwa Septemba 16 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Saalaam.
Soka CAF yateua waamuzi Watanzania
CAF yateua waamuzi Watanzania
Read also
