Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema anawaheshimu wapinzani wake, Dodoma Jiji ingawa anakipanga kikosi chake kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mechi dhidi ya timu hiyo.
Coastal na Dodoma zinatarajia kuumana kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga huku kukiwa na kumbukumbu ya mechi tatu baina ya timu hizo ambapo Coastal ilifungwa mchezo mmoja na kutoka suluhu mara mbili.
Akizungumzia hali hiyo, Mgunda alisema wataingia dimbani siku hiyo bila ya kutazama historia bali wao watatazama uhalisia uliopo na upinzani walionao msimu huu ambapo watahitaji ushindi kwa ajili ya kujisogeza juu zaidi katika msimamo na kujiengua kwenye wimbi la kushuka daraja.
Coastal iliyopo nafasi ya 10 ina pointi 28 sawa na Dodoma inayoshika nafasi ya 11 huku kila timu ikiwa imeshinda mechi saba, sare saba na kufungwa 10 huku tofauti yao ikiwa kwenye mabao ya kufunga na kufungwa.
“Mechi ni ngumu, tunawaheshimu pia Dodoma kutokana na kikosi na vijana walionao. Ni timu nzuri ingawa matokeo ni suala jingine na sisi tunajiandaa kwa ajili ya kuhakikisha tunapata ushindi ijapokuwa ni mechi ngumu kwetu.
“Tunafahamu kuhusu historia ya matokeo ya timu hizi lakini kama nilivyosema kiuhalisia mechi ni ngumu kutokana na kikosi cha wapinzani wetu na kuelekea mechi hii hatutazami historia, tutaangalia uhalisia na maandalizi ya kweli kama nilivyosema awali,” alisema Mgunda mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo.
Soka Mgunda: Tunawaheshimu Dodoma Jiji
Mgunda: Tunawaheshimu Dodoma Jiji
Related posts
Read also
