Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa Mtanzania, Novatus Dismas (pichani) amekamilisha dili la kujiunga na klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine akitokea S.V. Zulte Waregem ya nchini Ubelgiji.
Licha ya awali kuwepo kwa taarifa za nyota huyo kuwaniwa na timu za Middlesbrough na Southampton za England lakini jana duru mbalimbali za michezo Ulaya ziliripoti kuwa ni Shakhtar ndio iliyofanikiwa kunasa saini ya beki huyo.
Novatus anayemudu pia nafasi ya kiungo mkabaji ametajwa kutua kwa mabingwa hao mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu ya Ukraine, ikiwa ni siku moja imepita tangu timu hiyo itangazwe kupangwa Kundi H la Ligi ya Mabingwa Ulaya likiwa pia na timu za Barcelona, FC Porto na Royal Antwerp.
Ingawa bado haijawekwa wazi kuhusu mkataba wake na timu hiyo lakini imefafanuliwa kuwa amechukuliwa na timu kwa kandarasi ya muda mrefu.
Nyota huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa timu ya Taifa ya Tanzania, Stars, alipita katika timu ya vijana ya Azam kisha kupelekwa kwa mkopo Biashara United ya Mara mwaka 2020 kabla ya kurejea tena Azam ambayo ilimuuza Maccabi Tel Aviv ya Israel msimu wa 2020-21.
Soka Novatus huyooo Shakhtar
Novatus huyooo Shakhtar
Read also
