London, England
Mtu mmoja amekamatwa akihusishwa na wizi na uvamizi nyumbani kwa mshambuliaji wa Chelsea, Raheem Sterling (pichani) wakati wa fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar, Novemba na Desemba mwaka jana.
Katika tukio hilo lililotokea Desemba 3 mwaka jana wakati Sterling akiwa na timu ya England kwenye fainali za Kombe la Dunia, vitu kadhaa vya thamani viliibwa ikiwamo mapambo na vito pamoja na saa vyote vikiwa na thamani ya Dola 300,000.
Taarifa ya polisi ilieleza kuwa mtu huyo aliyetajwa kuwa na miaka 23 ameshitakiwa kwa makosa 33 ikiwamo kushiriki katika tukio la wizi na uvamizi kwenye nyumba na amewekwa rumande akitarajiwa kufikishwa mahakamani Septemba 21 mwaka huu.
Moja ya makosa anayoshitakiwa mtu huyo ni lile la uvamizi wa kwenye nyumba moja iliyopo Oxshott, kosa ambalo liliripotiwa kufanyika Desemba 3 mwaka jana.
Mara baada ya uvamizi huo kuripotiwa, Sterling aliondoka Qatar na kuwaacha wachezaji wenzake wa England kwenye fainali za Kombe la Dunia ili aweze kuwa karibu na familia yake.
Kimataifa Akamatwa akidaiwa kuiba kwa Sterling
Akamatwa akidaiwa kuiba kwa Sterling
Related posts
Read also