Na mwandishi wetu
Bondia wa ngumi za kulipwa, Hassan Mwakinyo amemshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa kurejesha matumaini ya mchezo wa ngumi visiwani humo.
Mwakinyo alikuwa ni miongoni mwa mabondia waliokuwepo Zanzibar katika pambano lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhusisha mabondia mbalimbali wa Tanzania bara na visiwani.
“Napenda kumpongeza Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyi ambaye anaweza asielewe ni kwa kiasi gani amerudisha matumaini makubwa kwenye mioyo ya wazazi wengi waliokwishapoteza matumaini juu ya vipawa na ndoto za watoto wao.
“Binafsi nina furaha kubwa sana juu ya uamuzi na hekima zako katika hii siku utakumbukwa daima, Viva Tanzania, Viva Zanzibar kwa umoja wa wachezaji wote wa Tanzania Bara na visiwani kwa ujumla tunayo ya kusema, nayo ni asante sana na Mungu akubariki,” alisema.
Takriban miaka 60 imepita tangu mchezo huo uzuiliwe miaka ya 1969 na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume kwa sababu za kiutamaduni lakini hivi karibuni kumefanyika mapambano, matamasha ya michezo kuonesha sasa Zanzibar wanarejea kimichezo.
Rais Mwinyi aliwahi kusema kuwa moja ya malengo yake ni kufufua michezo Zanzibar na tayari mafanikio yameanza kuonekana na wadau wakimuunga mkono kwa kupeleka mapambano.
Ngumi Mwakinyo ampongeza Rais Mwinyi
Mwakinyo ampongeza Rais Mwinyi
Read also
