Na mwandishi wetu
Azam FC imeeleza kuwa inajipanga vilivyo kumaliza maumivu waliyonayo ya kufungwa na Yanga kuelekea mchezo wao wa mshindi wa tatu dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa keshokutwa Jumapili.
Azam ilifungwa na Yanga mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kabla ya Singida nayo kusukumwa nje kwa matuta 4-2 na Simba katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja huo huo.
Ofisa Habari wa Azam, Hashim Ibwe alisema kuwa wanajisikia vibaya kwa kuwaangusha mashabiki wao kutokana na maandalizi waliyokuwa nayo ingawa anaamini kuanguka kwao ndiko kunakowapa morali kuelekea kutafuta ushindi katika mechi hiyo.
“Tunaamini kuanguka kwetu kwenye mechi ya nusu fainali ndiko kunakotupa morali vizuri kuelekea huo mchezo unaofuata, hatujaumia sana lakini imetuvunja kutokana na hali halisi lakini tuna imani ni namna bora ya kuanza kujitafuta zaidi, ukishateleza mara ya kwanza unakuwa na ufumbuzi zaidi uendako,” alisema Ibwe.
Mechi hiyo inatarajia kupigwa mapema majira ya saa 9.00 alasiri kabla ya fainali itakayowakutanisha mabingwa watetezi wa kombe hilo, Yanga dhidi ya Simba kuanzia saa 1.00 jioni. Mechi zote hizo zitapigwa Uwanja wa Mkwakwani.
Soka Azam FC kumalizia maumivu Singida FG
Azam FC kumalizia maumivu Singida FG
Read also
