Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane anasuburiwa kwa hamu katika klabu ya Bayern Munich baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo na leo Ijumaa huenda akafanyiwa vipimo vya afya.
Spurs hatimaye imekubali kumuuza mshambuliaji wao huyo tegemeo kwa ada inayodaiwa kufikia Pauni 86.4 milioni na mkataba wa miaka minne baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya klabu hizo mbili.
Bayern inafurahia ujio wa Kane kwa imani kwamba atakuwa suluhisho la safu ya ushambuliaji ya timu hiyo iliyoonekana kuyumba tangu kuondoka kwa Roberto Lewandowski aliyejiunga na Barca.
Msimu uliopita wa 2022-23, Bayern bila Lewandowski ilishindwa kutamba Ulaya na inaamini inahitaji kuimarisha safu yake ya ushambuliaji huku Kane akiaminiwa kuwa ataipa nguvu safu hiyo na kuipa mafanikio Bayern hasa Ulaya.
Awali Spurs walionekana kuwa wagumu kumuachia mshambuliaji huyo wakitarajia kupiga pesa ndefu lakini Kane mwenyewe alishaweka wazi msimamo wake wa kutaka kuihama Spurs huku Bayern ikiwa chaguo lake la kwanza licha ya kuwindwa na klabu za Man United na PSG.
Wakati mjadala baina ya klabu hizo ukiendelea, kocha wa Bayern, Thomas Tuchel alimfanya Kane kuwa chaguo lake la kwanza na angejiona ameumizwa kwa kumkosa mshambuliaji huyo.
Kane ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Spurs, anaondoka katika timu hiyo akiwa na rekodi ya kuifungia mabao 280 katika mechi 435 na ndiye mfungaji bora wa wakati wote katika historia ya Spurs.
Kimataifa Kane asubiriwa kwa hamu Bayern
Kane asubiriwa kwa hamu Bayern
Read also
