Na mwandishi wetu
Kiungo mpya wa timu ya Chippa United ya Afrika Kusini, Baraka Majogoro (pichani) ameeleza furaha yake ya kutua katika timu hiyo, akiahidi sasa ni wakati wa kuwapa furaha mashabiki na wadau wa timu hiyo.
Majogoro ameyasema hayo baada ya jana kutambulishwa rasmi na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
“Kwangu ni changamoto mpya katika maisha yangu ya mpira, lakini namshukuru Mungu kwa yote haya na sasa ninaangazia zaidi namna ya kuwapa furaha wapenzi wa soka na wadau na mashabiki wa Chippa United,” alisema Majogoro.
Majogoro aliyejiunga na Chippa akitokea KMC ya Dar es Salaam anapishana na beki wa kati Mtanzania, Abdi Banda aliyeitumikia timu hiyo msimu uliopita kabla ya hivi karibuni kutimkia timu ya Richards Bay.
Kiungo huyo aliyewahi kuzitumikia Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar ametua katika timu hiyo kuongeza nguvu kulingana na ushindani uliopo sasa katika Ligi Kuu uliopelekea Chippa kumaliza nafasi ya 14 na kuponea chupuchupu kushuka daraja.
Wachezaji wengine waliotambulishwa pamoja na Majogoro kwenye timu hiyo juzi ni Andile Fakude, Thabang Maloa, Senzo Nkwanyana na Lukhanyo July.
Soka Majogoro awaahidi furaha Chippa Utd
Majogoro awaahidi furaha Chippa Utd
Read also
