London, England
Klabu ya Everton inajiandaa kuzipiga bao Tottenham Hotspur na West Ham katika mbio za kumuwania beki wa kati ya Man United Harry Maguirre (pichani).
Maguire mwenye umri wa miaka 30 amepoteza uhakika wa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Man United na kwa sasa klabu hiyo inadaiwa kujiandaa kumpiga bei.
West Ham ilikuwa timu ya kwanza kujitokeza hadharani ikidai kumtaka beki huyo kabla ya Spurs kuingia katika mbio hizo na sasa Everton imeibuka huku ikidaiwa kutaka kuzipiga bao Spurs na West Ham.
Maguire mwenyewe hajatangaza anataka kujiunga na timu ipi kati ya hizo licha ya kutambua kwamba hana nafasi ya uhakika katika kikosi cha kwanza tangu msimu uliopita na tayari amevuliwa unahodha.
Msimu uliopita ulikuwa mgumu kwa Maguirre lakini aliendelea kuwa nahodha wa timu hiyo na kocha Erik ten Hag wakati wote alikuwa akimtetea akidai kwamba ana sifa zote za kuendelea kuwa nahodha wa timu hiyo licha ya kutokuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Maguire ambaye pia anaichezea timu ya England hata hivyo hatokuwa tayari kuendelea kubaki katika kikosi cha Man United wakati anatambua kwamba nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ni kama vile imeshapotea.
Kimataifa Everton yamgeukia Maguirre
Everton yamgeukia Maguirre
Read also
