Barcelona, Hispania
Baada ya mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe (pichani) kulipuuzia suala la kujiunga na Liverpool kwa mkopo, vita mpya ya kuisaka saini ya mchezaji huyo sasa imehamia katika klabu za Chelsea na Barcelona.
Klabu hizo mbili kwa sasa ndizo zinazotajwa zaidi baada ya kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti kunukuliwa hivi karibuni akisema kwamba timu yake ipo kamili hata kama itamkosa Mbappe.
Real Madrid imekuwa ikihusishwa na mshambuliaji huyo tangu msimu uliopita lakini ilimkosa na wakati wote Ancelotti amekuwa wazi kutoonesha kwamba anamhitaji kwa sana licha ya vyombo vya habari kulijadili sana suala la mchezaji huyo kwenda Real Madrid.
Mbappe pia hivi karibuni alikataa kujiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia licha ya klabu hiyo kumtangazia ofa kubwa ya Pauni 259 milioni ambayo ni rekodi ya dunia lakini ameipuuzia.
Kwa mazingira hayo kinachosubiriwa kwa sasa ni kuuzwa kwa Mbappe na Chelsea na Barca ndizo klabu zinazotajwa zaidi katika mpango huo.
Mkataba wa Mbappe na PSG unafikia mwisho majira ya kiangazi mwaka 2024 na ingawa hataki kuondoka PSG lakini klabu hiyo imemwambia kama anataka kubaki asaini mkataba mpya tofauti na hivyo ni lazima auzwe.
Kimataifa Mbappe azitesa Barca, Chelsea
Mbappe azitesa Barca, Chelsea
Read also
