Manchester, England
Klabu ya Manchester United ipo tayari kulipa Pauni 64 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 8 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Rasmus Hojlund (pichani) kutoka klabu ya Atlanta ya Italia.
Hojlund, 20, raia wa Denmark usajili wake ukikamilika atakuwa mchezaji wa tatu mpya kwenye kikosi cha kocha Erik ten Hag baada ya Mason Mount na Andre Onana.
Hojlund ametokea kuwa chaguo la kwanza kwa Ten Hag baada ya mpango wa kumsajili Harry Kane na Victor Osimhen kukwama na anaamini mchezaji huyo yuko katika umri sahihi hasa kwa kuwa Ten Hag anataka kuwekeza kwa wachezaji wa umri mdogo.
Awali klabu ya Atlanta ilitangaza kuwa ipo tayari kumuuza Hojlund kwa Pauni 77 milioni wakati Man United ilishikilia msimamo wa kutokuwa tayari kutoa zaidi ya Pauni 60 milioni kwa mchezaji huyo.
Man United hata hivyo inadaiwa kulegeza msimamo na imekubali kutoa pesa zaidi ikiwa na matarajio ya kumpata mchezaji huyo kabla ya siku ya mwisho ya kipindi cha usajili cha majira ya kiangazi.
Katika kinachoonekana kuwa Atlanta nayo ipo tayari kumuuza mchezaji huyo, juzi Jumamosi klabu hiyo ilimsajili mshambuliaji mpya, El Bilal Toure ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Hojlund.
Hojlund ametokea kuwa mmoja wa washambuliaji mahiri, msimu uliopita wa 2022-23, aliifungia Atlanta mabao tisa katika mechi 32 na kabla ya hapo akiwa Sturm Graz ya Copenhagen, aliifungia timu hiyo mabao 27 na pia ana mabao sita katika mechi sita za timu ya Taifa ya Denmark.
Kimataifa Man United, Hojlund kimeeleweka
Man United, Hojlund kimeeleweka
Read also
