Na mwandishi wetu
Timu ya Mashujaa ya Kigoma imefunguka kuwa imepunguza wachezaji wake wa awali na kubakiza wachezaji 16 pekee watakaoungana na wengine wapya kuipigania timu hiyo msimu ujao wa 2023-24.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Mashujaa, Edward Swai aliyefunguka kuwa hiyo ni mipango yao thabiti kuelekea Ligi Kuu Bara baada ya kupanda daraja mwishoni mwa msimu wa 2022-23.
“Tupo kwenye mipango ya kuhakikisha tunakuwa bora zaidi, tunaendelea kusuka kikosi chetu kikamilifu na tumewabakiza wachezaji takribani 16 katika wale tuliokuwa nao msimu uliopita, tumeongeza wengine kina Adam Adam, Zuberi Dabi na maingizo mengine ambayo tutayaweka wazi hivi karibuni,” alisema Swai.
Alisema kuwa kikosi chao kwa sasa kipo Zanzibar kikiendelea kujifua huku kocha wao mkuu, Mohamed Abdaalah ‘Baresi’ akihitaji maandalizi yafanyike huko kutokana na ugeni wa timu akiamini hapo ni sehemu pekee ya kuunda vyema kikosi cha mapigano ya ligi kuu msimu ujao.
“Kikosi kipo Zanzibar kutokana na malengo mbalimbali, ikiwemo kocha kuhitaji sehemu tulivu ili kusuka kikosi cha wachezaji wa zamani na wapya wanaoendelea kusajiliwa akiamini timu inahitaji utulivu na sehemu sahihi kama Zanzibar,” alisema Swai.
Soka Mashujaa yabaki na 16 wa zamani
Mashujaa yabaki na 16 wa zamani
Read also
