Texas, Marekani
Kiungo mpya wa Real Madrid, Jude Bellingham amefunga bao lake la kwanza na timu hiyo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Man United, mechi ambayo Real Madrid imeibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Alhamisi kwenye dimba la NRG mjini Houston, Texas, Bellingham alifunga bao hilo dakika ya tano ya mchezo huo mbele ya mashabiki 67,800.
Bellingham mwenye umri wa miaka 20 ambaye pia alikuwa akiwindwa na Man United, alicheza mechi hiyo kwa dakika 45 za kwanza ambazo zilimtosha kuacha alama kabla Joselu hajafunga bao la pili katika kipindi cha pili.
Nyota wapya wa Man United pamoja na timu yao kufungwa lakini walionesha uhai, mfano Mason Mount katika kipindi cha kwanza wakati kipa Andre Onana naye akicheza mechi yake ya kwanza alionesha umahiri alipookoa mpira uliopigwa na Joselu.
Ukiacha Onana, kocha wa Man United, Erik ten Hag pia alimpa nafasi kiungo wake mpya wa miaka 18, Kobbie Mainoo ambaye alikabiliana na Bellingham na viungo wakongwe wa Real Madrid, kina Luka Modric, Eduardo Camavinga na Aurelien Tchouameni.
Mainoo ambaye alikuwa kivutio katika mechi na Arsenal iliyopigwa mjini New Jersey, alishindwa kutema cheche mbele ya Real Madrid na kuishia kucheza kwa dakika mbili baada ya kugongana na Rodrygo.
Kimataifa Bellingham aiadhibu Man United
Bellingham aiadhibu Man United
Read also
