Na mwandishi wetu
Timu ya Singida Fountain Gate imeeleza kuwa kwa sasa haitatangaza usajili wa wachezaji wao wapya hadi siku maalum ya tamasha la timu hiyo, Singida Big Day litakalofanyika Agosti 2, mwaka huu.
Singida tayari imetambulisha wachezaji wawili, Joash Onyango kutoka Simba na Yahya Mbegu kutoka Ihefu huku ikielezwa tayari imemalizana na kipa Beno Kakolanya, winga Bernard Morrison na Morice Chukwu wa Rivers United ya Nigeria.
Ofisa Habari wa Singida FG, Hussein Masanza (pichani) ameeleza leo Alhamisi kuwa wanafahamu shauku kubwa iliyoko baina ya mashabiki na wadau wa soka juu ya usajili wao na sasa wamepanga kutoa shauku hizo zote siku ya tamasha hilo.
“Kimsingi tunafahamu juu ya kiu ya wadau kufahamu usajili wa Singida, nasi kwa sasa hatutambulisha tena mchezaji mpaka siku ya Singida Big Day itakayofanyika kwenye uwanja wetu wa Liti.
“Mbali na mambo mengi siku hiyo lakini utafanyika utambulisho rasmi sasa wa wachezaji wetu watakaoipambania timu msimu ujao kwenye michuano yote, hivyo watu wawe na subira kila kitu kitakuwa sawa siku hiyo, waje kwa wingi kushuhudia mambo mengi,” alisema Masanza.
Singida FG ni miongoni mwa timu mbili zitakazoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, nyingine ni Azam FC wakati Yanga na Simba zikitupa karata zao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Soka Singida FG kutotangaza wachezaji wapya
Singida FG kutotangaza wachezaji wapya
Read also
