Auckland, New Zealand
New Zealand imeanza vyema fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake Alhamisi hii ikiibwaga Norway bao 1-0 ingawa fainali hizo zimeathiriwa na mauaji ya watu wawili waliopigwa risasi na wengine sita kujeruhiwa.
Saa chache kabla ya kuanza fainali hizo milio ya risasi ilisikika na baadaye kuelezwa kuwa watu wawili waliuawa hali iliyozua taharuki miongoni mwa mashabiki na maofisa wa Fifa.
Hata hivyo muda mfupi baadaye, Fifa walieleza kuwa tukio hilo halina uhusiano wowote na fainali hizo zilizoanza rasmi kwa mechi hiyo.
Tukio hilo la risasi lilitokea mapema saa moja asubuhi katika eneo ambalo ujenzi ulikuwa ukifanyika lakini baadaye ilielezwa kuwa mtu aliyehusika katika tukio hilo ambalo halina viashiria vyovyote vya ugaidi, aliuawa.
Meya wa mji Auckland, Wayne Brown alisema maofisa wote wa Fifa wapo salama pamoja na timu zote za mataifa 32 kabla ya baadaye Fifa nao kutoa taarifa kwamba timu shiriki na maofisa wake wapo salama.
Haikuweza kufahamika mara moja kiini cha tukio hilo hasa kwa kuwa mhusika mkuu aliuawa muda mfupi baadaye ingawa mamlaka nchini New Zealand hazitaki kuona tukio hilo linaathiri kwa namna yoyote fainali hizo.
Ukiachana na mauaji hayo, New Zealand ambao ni wenyeji wa fainali hizo wakishirikiana na Australia, katika mechi hiyo ya kwanza bao lao lilifungwa na Hannah Wilkinson dakika tatu baada ya mapumziko.
Kimataifa Wawili wauawa kwenye Kombe la Dunia
Wawili wauawa kwenye Kombe la Dunia
Related posts
Read also
